Tuesday, January 11, 2011

How can we help?

Dear friends,
 I found this information on the famous MICHUZI blogspot. How can we help as Physio's? I am sure if we organise ourselves as APTA the child can benefit  from our vast knowledge.
The issue here is not money, I think we can teach the family and relatives how to take care of this lovely boy, including local made aids.
 Kindly email me for suggestions and ideas
Globu ya Jamii na Marafiki katika kumsaidia mtoto Abdully imefungua akaunti maalumu kama wadau mlivyoomba ili ikiwezekana asaidiwe yeye na baba yake. Vile vile msaada sio lazima pesa bali hata nguo, viatu na vitu vingine kwa ajili ya mtoto kama Abdully. Kutoa ni Moyo. Akaunti hiyo ni:
ACCOUNT NUMBER 014194
ABDUL MAHMOUD MIRROW
FEDERAL BANK OF MIDDLE EAST LTD
SAMORA BRANCH
DAR ES SALAAM
SWIFT CODE: fbmetztz
Kwa maelezo zaidi piga kwa Auntie Mariam
+255 754 280 495
Mtoto Abdully
Tuombe msaada kuwasaidia wenzetu ambao ni
mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu...
Ninakuomba kama mtanzania mwenzangu tupeane hamasa ya kupendana na kusaidiana sio katika sherehe za starehe tuu, zaidi siku hizi tuzidishe kusaidiana katika shida maana sasa shida zinazidi siku hadi siku.
Katika pitapita zangu, nimekutana na mtoto huyu Abdully mwenye ulemavu wa viungo huko Kaole, Bagamoyo. Kula kwake kwa taabu, haongei, ingawa anacheka akifurahishwa, na kulia kwa kupiga kelele akiudhiwa au akiwa na maumivu ingawa hawezi kuelekeza maumivi yako wapi.
Cha kusikitisha, mama yake mzazi amemkimbia mtoto na mume, baba nae ameanza kukata tamaa ya mwanae kwa kukosa muelekeo na msaada (support). Baba (Bw. Hamoud) anaishi na mama yake mzazi ambaye ni mtu mzima mwenye matatizo ya kiafya, macho na thyrod eshafanyiwa upasuaji nk... sasa Bw Hamoud ameacha shughuli za kutafuta fedha za kukimu maisha ili aweze kumlea kijana Abdul (4) ananza asubuhi kwa kumuosha, kumlisha kifungua kinywa..... mchana kumlisha anakula kwa taabu maana ulimi hauzunguki sawa sawa kama vile umepooza, na koo halimezi vizuri.... jioni anamsafisha na kumlisha.... maisha yamekuwa duni, kwa hivyo hata malezi ya Abdul yamekuwa magumu mno...
Alishauriwa ampeleke hospitali ya CCBRT, nae baada ya kwenda hapo alishauriwa ampeleke kwa physiotherapy kila wiki, tatizo la Bw Hamoud ni usafiri kutoka Kaole hadi msasani CCBRT ni wa daladala na mtoto mwenye ulemavu wa viuongo si mchezo... mlemavu wa aina hii anaweza kuwa na haja kubwa au ndogo mahali popote wakati wowote hata mkiwa ndani ya daladala huduma yake ngumu hapo ni mtihani...
Hapo CCBRT wanaweza kushinda kutwa kabla ya kupata huduma kipindi hicho cha kusubiri mtoto amebebwa au kupakatwa, chakula hakuna, na pahala pa kumlaza aweze anaglau kunyoosha viuongo hakuna. wahudumu wanapita na kumuangalia hapo katika foleni bila kumpa tamaa au hata nasaha. Jioni usafiri wa wa kubanana ndani ya daladala kurudi Bagamoyo, pikipiki hadi Kaole.... Baba Abdul kaishiwa nguvu ameshindwa. Wapo Kaole wanasubiri hatma ya Mwenyezi Mungu.
Abdul amepewa ki "baiskeli" cha mtoto (push chair) na akiwekwa hapo lazima afungwe na khanga ndio akae kwa usalama na kwa sasa anabanwa hapo....

Hivyo basi Kama kuna wasamaria
wenye huruma na hali hii, wanaomba:
1. Wheelchair ya kawaida Abdul akae
kwa usalama na awe na nafasi viungo viwe huru
2. Ushauri kwa kiafya
3. Ushauri wowote, na msaada wowote
utakaoweza kutoa afueni kwa Abdul na baba yake Hamoud
mpigie simu Hamoud
+255 757 652449 na +255 787 771566 kwa msaada au ushauri. Juhudi za kufungua
akaunti maalumu zinafanywa kwa wenye
kutaka kumsaidia mtoto Abdully
Mdau Dar
Mtoto Abdully anaomba msaada wako
Abdully akiwa amebebwa na nyaya yake
Abdully anasimama na kulala kwa shida...
(Picha na maneno kwa hisani ya MICHUZI

Ads 468x60px

APTA AGM WHERE? DAR ES SALAAM, MNH WHEN? 29TH OCTOBER- 2ND NOVEMBER 2012 BE SURE TO BE THERE!