Friday, October 22, 2010

Tujadili kuhusu aina hii ya wheelchair



Wadau tujadili kuhusu aina hii ya wheelchair.
Niliwahi kujadiliana na Fizio fulani hivi akaniambia "It is better than nothing". Hata mimi nakubaliana naye, zimesaidia kuwatoa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali toka sehemu moja hadi nyingine. Angalau.
Lakini mimi hofu yangu ni kuhusu "wasomi wa Afrika hasa Tanzania" , wheelchair hii ilibuniwa na mmarekani mmoja baada ya kuona shida wanayopata walemavu wa dunia ya tatu. Wheelchair hii imegawiwa maelfu kwa maelfu kwa wahitaji na wengine wametoka ndani ya nyumba zao kwa mara ya kwanza.
Je, hatujaweza na sisi kutoka na teknolojia rahisi??
Je, kwa wale ambao ziantumika maeneo yenu ya kazi, zina faida na hasara gani??
Kwa maelezo zaidi kuhusu aina hii ya wheelchair, bofya hapa
http://www.freewheelchairmission.org/site/c.fgLFIXOJKtF/b.4916275/k.BE91/Home.htm

3 comments:

Mathew said...

Yah! Nafikiri huyo mmarekani alikuwa na nia nzuri ya kusaidia watu kwa haraka kama binadamu yeyote mwenye huruma. Ni vizuri tukalisifu wazo lake la msaada wa haraka, ila pia tuna nafasi ya kushauri wasambazaji na watumiaji pamoja na mashirika, watu binafsi wanaoviagiza wakiwa na nia nzuri ya kusaidia walemavu wauone mwanga.
Kwa kuwa kila kitu kina faida na hasara zake basi tuna wajibu wa kushirikishana mawazo kama watu tunaokuwa karibu na walemavu zaidi.
Kwa uzoefu wangu kuhusu hicho kiti mwendo ni kwamba kinasababisha vidonda kwa haraka mno na pia huwa huteleza na kumfanya mtu aanguke kutoka kwenye kiti hicho kwa urahisi jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa zaidi kulinganisah na faida zake.
Ushauri: Kwa bahati nzuri kuna mashirika ambayo yameshirikiana na World Health Organization (WHO) na wamefundisha Watanzania namna ya kutengeneza viti mwendo vinayokidhi mazingira ya kwetu pamoja na mahitaji ya mgonjwa katika viwango vya kimataifa, wameweza pia kufungua vituo vya kutengeneza vitimwendo hivyo ambayo viko Arusha (Njiro Mobility)ambacho kipo ndani ya Sibusiso, Moshi kuna KCMC Wheelchair workshop, na Njoro Mobility Majengo. Vituo hivi vina wataalamu waliobobea katika kutengeneza viti mwendo kulingana na mazingira na tatizo mtu alilonalo.
Pia Tatcot KCMC wanatoa kozi maalum kwa ajili ya kutengeneza wheelchair na matumizi yake kwa ujumla, kozi hii inajumuisha kujua namna ya kujikinga na madhara mbalimbali yanayosababishwa na matumizi ya wheelchair.
Kwa maana hiyo basi tuna kazi kubwa ya kuielimisha jamii kuhusu matumizi ya kitimwendo chochote kile. Kumpatia mlemavu kiti mwendo bila kumpa elimu ya kutosha kunaweza kuleta madhara zaidi ya msaada ambao kingempa mlengwa.
Hata vinapoletwa nchini na makampuni au mashirika mbalimbali ya kutoa msaada ni vizuri kabla ya kusambazwa kwa wahitaji wawepo wataalamu (Physiotherapist, OT na Wheelchair technologist) ambao watatoa maelezo na elimu kwa walengwa.

Naishia hapo kama kuna swali usisite kuuliza kupitia ukurasa huu au e-mail(mateijo@gmail.com)

Fiziotherapisti said...

Tofauti kubwa nayoiona hapa yeye huyu anafanya mass production halafu anaenda kutafuta walengwa.Ingawaje vyuo na workshops zipo nafikiri wao wanasubiri oda au mnunuzi aje kununua lakini hatuna programu maalum ya kuhakikisha wahitaji wa wheelchair wanazipata.

Mathew said...

Hili si jambo la kwenda nalo kwa mazungumzo tu kama mjadala wa kisiasa, ni swala ambalo linahitaji utafiti pia. Utafiti utatusaidia kujua ni nini kimekosekana wapi na ni nini kifanyike ili kuziba pengo lililopo.
Kuna vikundi ambavyo viko tayari kutafuta wahitaji wa vitimwendo na kusaidia katika uwezekano wa kupata kiti hicho kwa bei nafuu na hata bure kwa wale wasiojiweza.
Kimojawapo ni KASI (Kilimanjaro Association of Spinally Injured)ambacho kipo mkoa wa Kilimanjaro na sasa hivi kina mpango wa kupanua huduma zake hadi mkoani Mwanza. Kikundi hiki kimeundwa na wahitaji wa vitimwendo na kinashirikiana na mashirika, vikundi, taasisi na mahospitali ili kuwafikia walengwa na kuhakikisha wamepata kiti mwendo kinachomstahili mlengwa kulingana na shida yake.
Tuanze mikakati ya kushirikiana na kuimarisha nguvu ambazo zipo tayari ili matunda yake yaonekane ili hata huyo anaefanya mass production aweze kurekebisha na kufanya mass production ya viti vyenye viwango vinavyokubalika badala ya hivyo ambayo tunafikiria havifai. Ni vizuri zaidi kama wadau tukafanya utafiti ambao utakuwa na vielelezo vya kutosha kuhusu madhara ya kitimwendo tunachofikiria hakifai tukilinganisha na kile ambacho tunafikiri kingefaa zaidi.
Tukiwashirikisha watumiaji watatupa uzoefu zaidi.

Ads 468x60px

APTA AGM WHERE? DAR ES SALAAM, MNH WHEN? 29TH OCTOBER- 2ND NOVEMBER 2012 BE SURE TO BE THERE!