Wednesday, October 27, 2010

Toka "Mzoeza viungo" hadi "Mfiziotherapia"

Tume toka mbali...jamani mama cheza, baba cheza, mzoeza viungo haya ni baadhi ya majina tuliyopewa sisi katika taaluma yetu. Nakumbuka kuna baadhi ya watu walikuwa hawawezi kuficha hisia zao pale waliposikia mteja akitamka, "Nimeandikiwa nikaonane na mama cheza"!


Ni kweli wengine lilitukera lakini tulikaa kimya tu. Wengine wetu walichukua muda kuwaelimisha wateja sisi ni nani. Naona sasa hata wale wataalam wa utumishi nchini wamelitambua hilo na sasa wametupa jina stahiki (kwa matazamo wangu) "mFiziotherapia". Tunashukuru.

Ninafikiri pia bado tuna kazi ya kuendelea kuwaelimisha waajiri, kada nyingine za afya na wateja wetu jinsi ambavyo tungependa tutambulike.

Kazi njema Fiziotherapisti!

No comments:

Ads 468x60px

APTA AGM WHERE? DAR ES SALAAM, MNH WHEN? 29TH OCTOBER- 2ND NOVEMBER 2012 BE SURE TO BE THERE!